Shilole ataja alichofanya ili kutoa AIBU wakati anafanya video ya Rayvanny ‘Natafuta kiki’.


Bongo fleva staa Shilole aka Bad Girl Shishi amesme alibidi anywe pombe kidogo ili atoe aibu ya kufanya video ya RayvannyNatafuta kiki
Kwenye ENews na Sammisago, Shilole amesmea “Mimi niliweka upendo na kuona nimsaidie mdogo wangu Raymond katika kazi yake ili iweze kutazamwa na watu wengi zaidi, ila kiukweli ilikuwa ni kazi mbaya sana kwangu na ngumu lakini nikaona maji nishayavulia nguo hivyo sina budi kuyaoga, nikamwambia Raymond wewe ni mdogo wangu sasa naanzaje kufanya haya mambo? Ilikuwa ni ngumu ikanibidi ninywe pombe kidogo ili niweze kuchangamka, kwani watu walikuwepo wengi nikawa naona aibu. Akaniambia hamna usijali hii kazi tu nisaidie tu, ikabidi nivae ile night dress na kuingia kazini“.
shilole-12 shilole-13
source;sammisago.com

No comments: