HAWA NDIYO WASANII BONGO WANAO ONGOZA KWA KIKI ZA KIMAPENZI

Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
Wakati Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ anaanzisha uhusiano wa kimapenzi na Zarinah Hassan ‘Zari’, yaliibuka maneno mengi.

Picha zilizovuja awali wakionekana kimahaba zilitafsiriwa kuwa, kuna video ambayo ingetoka ambayo Zari alitumika kama Video Queen ndiyo maana wengi wakajua kuna projekti imefanyika kati ya wawili hao.
Lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda huku kukionekana hakuna dalili za projekti yoyote kutoka, watu wakabadilika na kusema Diamond alikuwa akitafuta kiki tu, kwamba watu waone yuko kimapenzi na mwanadada huyo kisha iwe gumzo Uganda, Sauzi na Tanzania.
Kuonesha Kuwa walichokuwa wakiwaza watu ni tofauti na ukweli wa mambo, mara tukasikia Diamond kampa mimba Zari, mara Tiffah akazaliwa na hapo ndipo ilipobainika kuwa, wawili hao walikuwa na mapenzi ya kweli licha ya kuwa na sababu zao nyingine za kuwa ‘couple’.
Nay wa Mitego
Uhusiano wa wawili hao umewafanya wawe maarufu sana Afrika na hiyo imefanya Diamond kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupata tuzo mbalimbali kutokana na jitihada zake.
Wengine waiga Baada ya kuonekana kuwa uhusiano wa Zari na Diamond umezaa matunda, wapo wasanii wengine Bongo ambao wanaonekana kufuata nyayo.
nayChagga Baby
Nay wa Mitego juzikati ilidaiwa ana uhusiano na mwanadada Chagga Baby anayeishi nchini Marekani lakini chimbuko lake ni Uchagani, Moshi. Hatujakaa sawa tukasikia yule dogo wa Diamond anayesumbua na wimbo wake wa Aiyola, Harmonize naye kaomba nafasi kwa Huddah na mwanadada huyo naye anaonesha kumzimikia.
Wakati watu wakiendelea kufuatilia uhusiano uliopo kati ya Huddah na Harmonize, Mwanamuziki Ommy Dimpoz naye akafunguka kuwa, yuko in love na binti Muethiopia anayesoma Uingereza aitwaye Zerthun.
Ni mapenzi au kiki ya kimataifa?
homoHarmonize na Huddah.
Hilo ndilo swali ambalo mashabiki wengi wa wanamuziki hao wamekuwa wakijiuliza. Kwamba ni kweli imebainika kuwa, licha ya Diamond kutafuta kiki ya kimataifa kwa kuwa na Zari lakini wanapendana lakini je, ni kweli Harmonize anampenda kutoka moyoni Huddah?
ommy (1)Ommy Dimpoz
Ni kweli Chagga Baby na Nay wamezimikiana kikwelikweli?
Je, Dimpoz na yule Zerthun wake ipo siku wanaweza kufikia hatua ya kuitana mke na mume?
Inapokuwa ngumu kupata jibu la ndiyo kwa maswali hayo, ndipo linapokuja lile suala kwamba, wanamuziki hawa wanatafuta kiki za kimataifa kama alivyofanikiwa Diamond.
Zerthun
Anyway, hilo ndilo game la muziki na sarakasi zake. Kila mmoja anatumia mbinu anazojua kutafuta mafanikio, sisi yetu ni macho na masikio ila tunataka muziki mzuri. Kama wanapendana kweli, basi wasichezeane, wafanye kweli.

No comments: