Alichosema Harmonize kuhusu kufunya Kolabo na Raymond,Je anamwogopa?Hivi karibuni kwenye mitandao ya jamii kumekuwa na sekeseke kwa msanii wa bongo fleva,Harmonize kutoka kwa mashabiki wakitaka kujua kwanini hafanyi kolabo na mwana WCB mwenzake Raymond huku mashabiki wengi wakishilikia bango kuwa Harmonize anaogopa kufunikwa na Raymond.
Alipoulizwa kuhusu suala la yeye kutokufanya kolabo na Raymond,Harmonize alidai kuwa hana sababu ya kuhofia kufanya kazi na msanii mwenzake Raymond na kudai kwamba kama kuogopa angeogopa kufanya kazi na boss wake ,Diamond Platnumz.
Unajua kolabo ni biashara ya kubadilishana mashabiki,ndio maana mimi nilifanya na Diamond ili uwafikie watu wengi.Lakini ukija kwa Rayvanny na mimi,mimi ndiye nilianza kutoka kwa hiyo lazima nitengeneza misingi ili hata akija kufanya kolabo na mimi ajivunie,kihusu swala la kumwogopa kuwa atanifunika sio kweli,kama ndio hivo bhasi ningeogopa kufanya kolabo na Diamond maana anajua kuliko Rayvany na ana hits nyingi“,alifunguka Harmonize kwenye kipindi cha Enewz cha Eatv.

SOURCE;FAHAMU TV

No comments: