Header Ads

Tweet ya Diamond iliyozua gumzo twitter

Asubuhi ya leo Diamond Platnumz alichukua headlines katika mtandao wa twitter baada ya ku-tweet kuwa anajisikia kuachia nyimbo siku ya leo.


Kitu ambacho kilizua shahuku kubwa kwa wapenzi wa burudani ambao ni watumiaji wa mtandao huo na kusababisha tweet hiyo kufikisha likes 123 na retweets 47 ndani ya muda mfupi tu.
Uongozi wa Diamond Platnumz uliahidi kuwa endapo video ya msanii huyo ya “Kidogo” ambayo kafanya na P Square ikifikisha viewers million 5 katika mtandao wa Youtube basi watatoa zawadi kwa mashabiki wao kwa kudropisha ngoma nyingine tena. Na hadi sasa video ya Kidogo ina viewers zaidi ya 4,763,765.
Zipo commenst kutoka kwa mashabiki zilizomzuia Diamond kuachia ngoma leo kwa madai ya kuupisha msimu wa Fiesta ila lolote linawezekana, cha msingi ni kuendelea kusubiri na kujua kipi kitatokea.

No comments: