SHILOLE KIUNO ATOBOA SIRI JINSI ALIVYOWEZA KUREKODI VIDEO AKIWA BILA KUFULI


Shilole Afunguka 'Sitaki Mzee Nitamburuza, Nahitaji ‘Dogo Dogo’ Ili Anipetipeti'
Mwanamuziki wa Bongo flava ambaye anavibwanga kila siku kwenye mitandao ya kijamii kwa skendo ya k..Mwanamuziki wa Bongo flava ambaye anavibwanga kila siku kwenye mitandao ya kijamii kwa skendo ya kutoka na vijana walio chini ya umri wake amefunguka nakusema asipangiwe ni nani wa kuwa naye.


Akiongea mbele ya kamera za eNEWZ, Shilole amesema mashabiki wanahitaji yeye awe na Mzee lakini yeye haoni haja ya kuwa na mzee kwakuwa hawawezi ‘kumpetipeti’ nakuwataka wamuache achague anachotaka kwakuwa nyumbani ni Zuwena na jukwaani ni Shilole.
“This is my life, Nikiwa nyumbani ni Zuwena nanikiwa kwenye TV ni Shishi, maisha yangu mimi ya nyumbani au maisha yangu binafsi wao yasiwausu sana ninaangali upendo wangu upowapi. Nikisema niangalia mashabiki nini wanacho taka wao wanataka niwe na Mzee, Sasa maisha yangu nianze kuwa na mzee nianze kumburuza! Mimi ninahitaji kijana aanze kunipetipeti” Alifunguka Shilole kwa madaha.
Lakini Shilole alimalizia kwakusema kuwa mpenzi wake mpya wa sasa ni msanii wa muziki na wala hajawahi kubahatika kuwa na mpenzi ambaye ni dakitari au mwalimu, Bali ana nyota ya kukutana na wasanii tu.
eNEWZ ilitaka kupenyeza zaidi kutaka kujua kisa cha msanii mkubwa kama yeye kuonekana kama video queen kwenye video tatu hadi sasa ikiwa nipamoja na video ya Manfongo ‘Hainaga ushemeji’, Darassa ‘To Much’ na Rayvan ‘Natafuta kiki’. Shilole aliweka wazi kuwa kuonekana kwenye video zote hizo ametokea kwakuwa anaurafiki na wasanii hao akaona asiweke u staa kwakuwa hata yeye Alisha wahi kuwa video vixen.
Akifafanua zaidi kwenye muonekano wake katika video ya Rayvan, Shilole amesema hakuvaa chochote ndani zaidi ya nightdress, hivyo ilimbidi atupie kileo ili aweze kufanya scene hiyo.

No comments: