Header Ads

SIMBA YAZIDI KUPELEKA MAUMIVU JANGWANI

SIMBA YAZIDI KUPELEKA MAUMIVU JANGWANI
SIMBA YAZIDI KUPELEKA MAUMIVU JANGWANI


Kikosi cha Simba kimezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City FC.

Mabao ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi, Asante Kwasi na John Bocco.

Mbeya City wamejipatia bao lao kupitia kwa Frank Ikobel na kuufanya mchezo umalizike kwa idadi hiyo ya mabao.

Simba wamefikisha alama 55 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga walio na 47.

Mpaka sasa Simba imeshacheza jumla ya michezo 23 huku Yanga ikiwa na 22.

No comments: