Header Ads

SIMBA NJIA NYEUPE UBINGWA MSIMU HUU

Timu ya Simba imejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba imefikisha pointi 55 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimano alama nane juu ya Yanga walio nafasi ya pili.

Emmanuel Okwi aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 16 baada ya shuti la John Bocco kuzuiwa na mlinda mlango Owen Chaima kabla ya kumkuta Mganda huyo.

Simba iliendelea kulishambulia lango la City na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Asante Kwasi dakika ya 32 baada ya kupokea pasi ya Shiza Kichuya.

Winga Frank Ikobela aliifungia City bao hilo kwa kichwa dakika ya 34 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Majaliwa Shaban kabla ya Bocco kuipatia Simba bao la tatu dakika moja baadae baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Shomari Kapombe.

Kwasi alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 70 baada ya kupata maumivu kwenye mguu.

City iliwatoa Babu Ally, Danny Joram na Victor Hangaya nafasi zao zikachukuliwa na Hamidu Mohammed, Mohammed Samata na Geofrey Muller.

Simba iliwatoa Kwasi, Bocco na Nicholas Gyan na kuwaingiza Mohammed Hussein na Laudit Mavugo na James Kotei.

No comments: