Header Ads

Lwandamina aacha maumivu Yanga

Lwandamina alitangwaza siku chache zilizopita kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Zesco United ya nchini Zambia kuchukua mikoba ya Tenant Chembo.
Mzambia huyo ambaye ameondoa Yanga kinyemela,  aliipa ubingwa klabu hiyo msimu uliopita wa 2016/2017 kwa faida ya mabao kutokana na kulingana pointi 68 na Simba.
"Sina taarifa rasmi za kuondoka kwake lakini ni wazi inafahamika kuwa baba akiondoka kwenye familia lazima kuna hali ambayo sio ya kawaida itatokea, naomba ieleweke hivyo kwa sababu sipendi hilo kuliongelea sana.
"Uongozi unaendelea na mengine, siku yoyote utatoa tamko, lakini tutajitahidi kuhakikisha timu inaendelea kuwa kwenye kasi ile ile ya ushindani, " alisema kocha huyo msaidizi.
Akizungumzia utofauti wa pointi uliopo baina yao na Simba mara baada ya kutoka sare bao 1-1 na Singida United juzi, Nsajigwa alisema pointi tano sio nyingi sana kwa kutizama michezo iliyosalia.
"Tuna nafasi ya kutwaa ubingwa, bado tuna mechi 8 mbele, ukiangalia pointi hizo ni mechi mbili tu, kama ingekuwa zimebaki mechi mbili msimu kumalizika tungesema nafasi yetu ni finyu.
"Nguvu yetu tunailejeza kwenye michezo inayofuata ili kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu, " alisema kocha huyo ambaye aliwahi kuichezea Yanga enzi zake kwa mafanikio

No comments: