Christian Bella kutikisa Miss Indian Ocean Dar agosti 12.

KING Of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuwa miongoni mwa mastaa watakaotoa burudani kabambe katika Shindano la Miss Dar Indian Ocean litakalofanyika Agosti 12, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Msasani Club jijini Dar.
Akizungumza na Showbiz, mratibu wa shindano hilo Grace Shija alisema kuwa, tayari kamati imejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mmoja atakapofika kwenye shindano hilo apate burudani ya kutosha.

Wakitabasamu.
“Tumejipanga vizuri kabisa, shindano litasindikizwa na mkali wa miondoko ya Dansi nchini, Christian Bella na wakali wengine wengi. Nafikiri kila atakayehudhuria ataburudika ipasavyo kwani hata warembo watakaoshiriki nao wapo vizuri na mazoezi ya kasi yameshaanza kuhakikisha hatukosei kitu,” alisema Grace.
Washiriki wa shindano hilo ni Amina Mohamed,Martha Melle, Sharifa Rajab, Eva Sebastian,Aisha Haruni, Magreth Mwambi Rachel Zachari, Flora Robert, Elizabeth Julius na Agness Johanes.
Shindano hilo limedhaminiwa na gazeti pendwa namba moja kutoka Global Publishers la Amani. Wadhamini wengine ni Wolpersytlish, Atsoko na Clouds FM.

Christian Bella kutikisa Miss Indian Ocean Dar agosti 12. Christian Bella kutikisa Miss Indian Ocean Dar agosti 12. Reviewed by mkundi tv on 2:36:00 AM Rating: 5

Follow by Email